Donda Langu Poem by Hesbon Nyamweya

Donda Langu

Roho yangu maskini Mungu wangu....
Hiki kidonda imeenea ndani yangu chunguchungu.....
Furaha yangu katolewa kafara kwenye dungudungu.....
Huku fedheha yakinifanya kununu...
Tahayuri jamani nimezwe na ulimwengu....
Maisha yakisonga kama vunjajungu....
Niwe mgeni wa nani maisha huu uvurungu....
Ninayepoteza kwa urahisi changu.....
Sio tu mangamungamu bali kizunguzungu...
Huku moyo wangu ikitandishwa mwiba wa nungunungu....
Nilie aje mpenzi naumia mwenzangu...
Rudi nyota yangu, niko wako pingu...
Nipe nasibu wangu tena nitabasamu.
Maana kutowepo kwako ni donda langu.

Ni jana nilikua wako mwaridi na nyota
Ni jana penzi letu lilikua barazahi wangu sista....
Sio kitambo nilikua wako kimetameta...
Fungo letu sasa imezorota....
Na moyo wako ukatia ukuta....
Kumbukumbu letu kwako umevuta....
Kwa donda langu umekua kigongota...
Chozi langu kwako sio hoja...
Na huzuni wangu kwako ni masihara...
Wangu mahaba, rudi niponye donda langu.

Kipenzi bado niko hapa nangoja...
Nikitaraji hatujaunguza yetu daraja...
Bado kumbukumbu letu lanipa faraja...
Hata kwa simu uwe mteja...
Bado nitazidi kukungoja
Picha akilini bado kwangu tafrija....
Hata kama kukupoteza ni mauja.
Natumai subira italeta kwangu natija...
Maana sina lingine ila wewe moja..
Nikijua karibuni tutakua pamoja..
Tukikumbatiana na kupigana pambaja....
Maana wewe na mimi ni kitu kimoja...
Kwa hivyo rudi niponye yangu donda.

...............................END..................

READ THIS POEM IN OTHER LANGUAGES
Close
Error Success